Monday, January 14, 2008

Mambo ya Dathalama- chuna buzi kwa kwenda mbele!!

Siku ya leo nina tukio moja nililoshuhudia kwa macho yangu siku ya mwaka mpya,Unajua saa nyingine inabidi uwe mdadisi kweli,Nilitia miguu sehemu moja ili nione yanayoendelea duniani, haa kweli duniani kuna mambo!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Niko kwenye kijibaa kimoja mitaa ya uswahilini na scene ninayoishuhudia mbele yangu ni kama ndoto vile. Yupo dada mmoja amejipiga mkorogo wa kueleweka na kwa kumtazama taratibu umbo lake na sura- mashalaah- si haba, amekaa peke yake anakunywa coke na kama meza mbili toka hapo alipokaa kuna jamaa mmoja hivi, kwa kumcheki chapchap kwa jinsi alivyovaa- anaonekana 'wakuja', huyu jamaa anapiga 'kili' baridi na haishi kumkodolea huyo dada aliye pembeni yake.
"Vipi kaka? mbona unaniangalia sana? umenipenda?" anauliza mwanadada bila haya kwa sauti kubwa tu huku jicho akilizungusha. Jamaa anaonekana wazi amepatwa na mshtuko, hakutarajia swali kama hili. "Aah, mtoto kama wewe kila mwanaume lazime akupende", jamaa anajibu huku akitoa tabasamu la mashaka. "Njoo basi tukae wote hapa mezani kwangu" na bila kusita, jamaa anahama na 'kili' yake na kuungana na mwanadada huyo.Kutokana na accent ya jamaa na intro yake kwa mwanadada niliyoiskia nagundua kuwa ni mfanya biashara wa mifugo toka mkoa fulani wa kanda ya ziwa.
'Waiter' mwanadada anaita kwa sauti na mmoja wa wahudumu bila kuchelewa anakuja kumsikiliza "Niletee chupa kubwa ya amarula" ,sikumsikia mshkaji akikaribisha kinywaji nikadhani labda atalipa mwenyewe, mind you mwanzoni alikua ana mwendo wa coke! Huku maongezi yakiendelea na mshikaji, namuona mdada akipokea simu na kumueleza mtu mwingine mahali alipo, baada ya kama dakika ishirini hivi anakuja dada mwingine na alipokaa tu kwenye kiti bila hata kukaribishwa, akaagiza kamzinga kadogo ka konyagi na bitter lemon.Dada mwenyeji sasa aliniacha hoi alipokuwa akitoa intro "Shemeji yako huyu" Jamaa huku akitabasamu akasema "Hee, yamekuwa hayo tena?" Akaulizwa "Unashangaa nini? kwani wapenzi si huwa wanakutana sehemu kama hizi pia?" Baada ya masaa kadhaa nashtushwa na sauti kubwa ya mdada wa kwanza, " Jikooooni", mtu wa jikoni alipofika akatoa order " Tuletee kuku mzima wa kuchoma na ndizi nne, naomba ufunge kwa kuwa tunaondoka muda si mrefu"
"Sasa mpenzi niambie umefika hoteli gani ili nikishaonana na mama nikutafute jioni? au utakuwa hapa hapa?" Mshkaji anaulizwa na yule dada wa kwanza, namsikia akitaja jina la guest moja ya Sinza ambayo mwanadada anaonekana kuifahamu lakini kabla hajaondoka anamwambia kuwa hana dola na anaomba mshkaji amuwekee dola tano ili mawasiliano yawe rahisi, jamaa akaingia king. Mzinga wa mwisho kabisa niliousikia ni "Sasa niachie kabisa basi hela ya taxi,si unajua daladala za Sinza zilivyo tabu jioni?" aflu kumi ikatoka shwaa!
Jamaa alipoletewa bill jicho lilimtoka kichizi, nilidhani angeanguka pale, nilimsikia tu akiongea kilugha mwenyewe baada ya kulipa lakini nahisi ilimbidi aguse mtaji kulipa hilo deni."Ndio mkome kuparamia mashankupe ya mjini" alisikika akisema mhudumu mmoja wa kike wa baa hiyo.
Sijui hata wewe ulishayashuhudia hayo.Ni sooo
Nakutakia kila la kheri mkuu wangu
Sibo

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home