MAADILI YA VIONGOZI WETU..
Hii ni maada ambayo imetolewa na mdau wetu toka Chuo kikuu cha Ardhi jiji Dar es salaam....
Na Seleman kassase.
Hi mwana maadili ya uongozi yaliisha enzi za mwalimu Nyerere. Subiri nikupe sakata la DAWASCO ni hivi kwa mujibu wa DAWASCO waziri wa wizara ya maji Dk Shukuru Kawambwa ni mmoja wa wadaiwa sugu, ktk kujitetea waziri Kawambwa alidai kuwa huwa DAWASCO wanampelekea bili tu lakini maji huwa hapati so akaacha kulipa.( makubwa haya mzee). Najiuliza hv km ni kweli DAWASCO walikuwa wakimpa bili tu bila huduma why asichukue hatua dhidi yao coz yeye ndie mwenye dhamna ya kuhahakisha wananchi wanapata huduma bora ya maji, sisi kama hao DAWASCO wamethubutu kumfanyia hivyo yeye kwa walala hoi itakuwaje??? mimi naona ni afadhali ya kina chifu Mangungo kuliko hawa wetu wa sasa. toka lini nchi ikaendelea kwa kupata mrabaha wa 3% kutokana na madini, eg Norway wanachukua 75% , wapi na wapi hapo. Je ni kweli waafrika tumelaaniwa. THE BEAUTIFUL ONE ARE NOT YET BORN kila mtu huweka pesa mbele hata wanachuo ss wameharibika. Hivi ni kweli tunaimport hata stick za meno mhh.
Wadau kama nitakuwa nimekuudhi niwie radhi, rejea songs of lawino and okol, wakoloni walipokja wakasema majina ya kiaafrika ni ya kishenzi yasiyokuwa na maana, sisi ni kwa nini tunaendelea kutumia majina ya kizungu na kiarabu, walai hawa jamaa hawatakuja kutuheshimu mpaka tukapojikomboa kifikra. Majina km Kassase, Ambele, Macha,Masanja, Njagamba, ni mazuri kabisa.
Sawa basi kama wazazi wetu waliteleza naomba vijana wenzangu vizazi vyetu tuvipe majina ya asili tuondoe chembechembe zote za ukoloni. kiongozi bora ni yule anaekubali kuongozwa na kukosolewa, naomba maoni yenu.
0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home