Friday, December 7, 2007

WOGA WAZAA MAWAZO

Leo naamkia uzazi. Uzazi wa mawazo. Mawazo. Mawazo.Upo umuhimu mkubwa sana wa sisi kama binadamu kujielewa. Kujielewa kutatusaidia kutatua matatizo yetu mengi. Matatizo ya kiutamaduni. Kisiasa. Kijamii. Na kadhalika. Kulielewa ni muhimu sana.Kujielewa ninakokuzungumza hapa ni kule kufahamu kuwa ndani mwako yapo mawazo ambayo usipoyagundua yatakufa na wewe. Wewe unayo mawazo muhimu sana kwa ajili ya maendeleo ya watu wanaokuzunguka. Bahati mbaya ni kwamba mawazo hayo yanakusubiri wewe uache woga. Useme. Ueleweke unawaza nini.Mengi ya matatizo yetu hayako huko tunakodhani. Si unajua mara zote huwa hatupendi kuwajikia matatizo?Chanzo cha matatizo yetu kiko katika fahamu zetu wenyewe. Lakini ajabu ni kwamba watu wengi tunajua sana kuzungumzia udhaifu wa wengine. Tunajua kuchambua hoja za wengine. Tunajua kupuuza vya wengine. Tunajua kulalamika. Kusononeka. Lakini kumbe kufanya hivyo hakuwezi kuleta mabadiliko ya kweli.Hivi sasa wananchi wanalalama. Serikali imefanya hiki. Serikali. Serikali oooh. Serikali. Serikali uuuh. Serikali. Lakini wanasahau kuwa ni wao wenyewe ndio ndio "walioiajiri" serikali hiyo. Ubora ama udhaifu wake, wa kulaumiwa ni wao wenyewe.Huwezi kulalamika leo wakati jana ulibadilishana kura kwa kopo la mbege. Ulikubali mwenyewe, kuuza haki yako kwa kutokujielewa wewe, unacholalamikia ni nini? Narudi kwenye hoja.Ni rahisi sana kukosoa mawazo ya wenzetu, kuliko kuonyesha msimamo wetu kwa kuzalisha mawazo yetu wenyewe na kuyasimamia.Hima tuamke. Tuzae mawazo.Mawazo ni mawazo. Toa mawazo yako waziwazi. Sema unachofikiria. Zaa mawazo. Kwa sababu hakuna mwingine mwenye mawazo yanayofanana na yako. Usilalamike sana. Weka wazi mbadala ulionao. Usijidharau. Sema unachowaza, utusaidie.Hapo tutaanza kuona tofauti.
Na. RAITON AMBELE

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home