Friday, December 7, 2007

MAHAKAMANI SI SEHEMU YA MIPASHO

Mahakamani sio sehemu ya mipasho, Mahakamani sio uwanja wa vitisho, ni sehemu inayopaswa kuheshimiwa na watu wote bila kujali vyeo vyao au umaarufu walio nao katika jamii, ni sehemu ambapo haki hutolewa katika misingi ya kufuata sheria na kanuni zilizowekwa, hivi ndivyo tunavyopaswa kujua.Nimeamua kusema hivi kwa kuwa naiona hatari kubwa inayokuja mbele yetu sisi kama wananchi wa taifa linalodai kufuata misingi ya democrasia ya kweli inayofuata taratibu chanya tulizojiwekea ingawa nyingine nyingi bado zinahitaji marekebisho ya mara kwa mara ili ziendane na mabadiliko ya wakati uliopo.Hivi karibuni Wakili msomi mwezangu Fatma Karume alidhihirisha kwa umma wa Watanzania kuwa ni jinsi gani ilivyo rahisi kwa mtu aliyeko madarakani au mtu anayesafiria nyota ya cheo cha baba au mama au wanafamilia kama tiketi katika kufanya jambo lolote hasa linapokuja swala la kufuata kanuni na maadili ya kazi husika kwa mfano hii ya uwakili.Wakili ni mtu ambaye anatakiwa awe mfano bora si tu kwa mteja bali ana wajibu mkubwa kwa mahakama na taifa lake katika kuhakikisha kuwa sheria na taratibu zinafuatwa ili haki iweze kutendeka, Ni ukweli usiopingika kuwa wakili aliye makini anajua nini anachotakiwa kukifanya ili haki iweze kutendeka si tu kwa kumtetea mteja wake bali kwa ajili ya kutetea haki ,kwa mfano wakili anapofanya makosa ya kitaaluma kuna kamati za maadili zinazoshughulikia tatizo husika, katika kukazia hili sitasita kumtaja Wakili msomi mwenzangu Dr Masumbuko Lamwai ambaye hivi majuzi alipewa adhabu ya kufungiwa kufanya kazi kama wakili kwa muda wa mwaka mmoja na kuamuliwa kumlipa mteja wake kiasi cha shilingi milioni mia moja na ishrini kutokana na makosa ya kiutendaji katika taaluma yake, hii inakuwa kama fundisho kwa wote wasiofuata maadili ya kazi zao, wapo wengi waliokwisha kukumbwa na adhabu kama hizo ila kwa kuwa pengine hawana majina ndio maana hukuwasikia lakini walioko ndani ya fani husika kitu kama hicho ni cha kawaida sana...usishangaeSijajua bado ni adhabu gani anayostahili kupewa mtu anayetoa vitisho kwa mheshimiwa Hakimu au Jaji eti kwa kuwa tu yeye ni mtoto wa kigogo fulani,sijui, lakini ninachojua ni kwamba inapofika wakati ambapo watu waliopewa dhamana katika kuhakikisha kuwa haki inatendeka wanapewa vitisho katika utekelezaji wa majukumu yao basi ujue kuwa tumefikia mahali pabaya.Sijui nia ya mhusika inakuwa ni nini?je haki itolewe kwa kuwa yeye kasema?, katika mazingira kama hayo hata kama haki itatolewa kihalali pasipo kuwa na mizingwe yoyote bado kutakuwa na malalamiko yasiyokwisha kutoka upande wa pili kwa kuamini kuwa penginne uamuzi uliotolewa ulifuata misingi ya upendeleo kutokana na vitisho vilivyotokea....hii ni hatari ya pekee.Vipo vyombo vingi vilivyowekwa kisheria katika kufuatilia nyendo na malalamiko yote yanayohusu utendaji au tuhuma zozote katika taaluma husika, kama nilivyotaja hapo awali kuwa ipo kamati ya maadili ambayo hukaliwa na majaji watatu wa mahakama kuu , vipo vyama vya mawakili,wapo PCB ambao pia hushughulika tuhuma kama hiyo iliyotolea na Wakili fatma, na vyombo vinginevyo lukuki lakini katika mazingira ya kesi ya Fatma hatujasikia chochote kutoka kwa vyombo vinavyohusika, hapa napatwa na maswali mengi, je vyombo hivi havikushirikishwa?kama vilishirikishwa vimetoa uamuzi gani?na kama havikushirikishwa ni kwa sababu gani?. ni vyema wazalendo wenzangu mkajua kuwa haki haiwezi kupatikana kwa kuongea na waandishi wa habari peke yake au taratibu za kitaaluma haziwezi kukiukwa kwa sababu tu eti jambo husika limezungumziwa katika kituo fulani cha redio.....Mahakama haipo hivyo na ndio maana huwezi ukakuta jaji au hakimu au wakili aliye makini akizungumza ovyo ovyo katika vyombo vya habari, sio kwa sababu kuwa hawana uhuru wa kuongea bali kwa sababu maadili ya kazi yao hayawalazimishi kuongea ongea ovyo au kusimama katika majukwaa ya kisiasa na kuanza kufanya kampeni ili kesi zao zishinde.Maadili ya kazi ya uwakili kwanza hayamruhusu wakili yoyote kuzungumzia kesi ambayo anaiendesha kwa mtu mwingine ambaye si mteja wake kwani kwa kufanya hivyo atakuwa anatoa siri za mteja au wateja wake. Wakili anawajibu mkubwa wa kutunza siri za mteja wake.Taratibu hizi hazipo tu katika kazi ya uwakili bali hata katika nyanja nyingine kwa mfano kamati mbalimbali zinapoundwa hazitakiwi kuzungumza chochote nje ya kamati husika kabla maamuzi hayajafikia mwisho, hata hivyo si kila mtu ndani ya kamati hiyo anakuwa ni msemaji bali kutakuwa na msemaji ambaye mara nyingi huwa ni mwenyekiti au mtu yoyoye aliyepewa mamlaka ya kutoa matokea ya kamati husika, huu ni utaratibu uliozoeleka na ambao hata katika vikao vya harusi hutumiwa....Hatari iliyoko mbele yetu katika sekta ya Mahakama ni kubwa kwani kama hatua za kinidhamu hazitachukuliwa dhidi ya wanaokiuka maadili ya kazi zao tutakuwa na idara ambayo inaendeshwa kwa kufuata amri ya mtu mwingine kwa kuwa eti yeye ndiye binadamu zaidi kupita wengine ,siasa ni siasa na taaluma ni taaluma, tusichanganye vitu hivi viwili. ukitaka kuhakikisha ukweli huu jaribu kuchunguza kiwango cha elimu anachotakiwa mtu kuwa nacho ili aweze kupata kiti cha ubunge kisha linganisha na kiwango anachotakiwa kuwa nacho hakimu au jaji ndipo utakapojua kuwa siasa ni siasa na taaluma ni taaluma.Kuzunguka katika vyombo vya habari za burudani na kuanza kutoa shutuma dhidi ya mtu ambaye ungepaswa kwenda kumshtaki kwa bosi wake haiwezi kusaidia chochote kwani tuhuma hizo haziwezi kushughulikiwa kwa kuwa vielelezo ulivyo navyo hukuvifikishwa panapohusika ili mtuhumiwa aweze kuchukuliwa hatua za kinidhamu kupitia vyombo vinavyohusika na taaluma yake. Kwa mfano, leo hii siwezi kukurupuka na kuanza kumtuhumu mchezaji wa simba Juma Kaseja kwa utovu wa nidhamu katika michezo kupitia vyombo vya habari wakati nikijua kuwa tatizo hilo linaweza kushulikiwa vizuri na TFF vinginevyo itokee sababu kwamba sizijui Ofisi za TFF lakini hata hivyo bado naweza kuwauliza watu na wakanielekeza zilipo ofisi hizo...simple like that...,Vinginevyo tutakuwa tunajenga wanataaluma waliokaa kisiasa zaidi kuliko kufuata taaluma zao,ebu jaribu kufikiria, daktari awe kisiasa zaidi,hospitali nazo ziwe kisiasa zaidi je mgonjwa atatibuiwa na kupona kweli? sikatai kuw wapo walao rushwa katika idara ya mahakama lakini tuhuma hizo haziwezi kuwa kigezo cha kutofuata taratibu katika kuhakikisha mafisadi wa haki za watanzania wanakamatwa na kuchukuliwa hatuaKwa wanaojua taaluma zao wanajua kuwa wachimbao mashimo kwa ulimi hawawezi kuyafukia watakapotakiwa kufanya hivyo....Huu ni mtazamo wangu tu .....naomba msijenge chuki

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home