Tuesday, December 11, 2007

SERIKALI YETU IMEWAHIFADHI MAFISADI NA KUENDELEA PIGA GUMZO LA KAMATI ZISIZO NA NGUVU KISHERIA.




Sasa labda lini sisi kama Tanzania tunaweza piga hatua ya kimaendeleo kama nchi?Hili ni swali ambaloo hata viongozi wanadai kuwa hawana jibu sahihi Haya je kuhusu suala la mikataba nalo viongozi watasema hawana jibu je ni nani alie ingia hiy mikataba ni raia asikwenda shule au ni hao hao viongozi, je walipokuwa wakitia sahihi hiyo mikataba hawakuisoma kuwa ina maanisha nini? Au zote ni propaganda tu kwa wananchi na wao washakula chao.Je kamati hizi zinazoenda kagua mikataba ya madini kwa tujiulize ni kamati ya Bunge au ni kamati ya kumshauri rais juu ya mikataba ya madini maana kama ni ya Bunge basi itakua heri maana itakua na nguvu kusheria na kama ni ya rais haina maana yoyote maana haitaweza badilisha lolote juu ya mikataba mpaka rais atakapoo toa tamko haya yetu macho na masiki baada ya miezi mitatu ya kupitia mikataba hiyoo.

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home