MWANAMKE NI "VICTIM" BILA KUJIJUA!!
KILA MTU NA FANI YAKE DUNIANI HAYA KAZI KWENU.!!
Leo na-promote Uanamke….
Wiki iliyopita nilikuwa kwenye sherehe za kamuagano (Sendoff) na Kesho yake nikaenda kwenye sherehe za ndoa..….kama mjuavyo penye wengi ndio mahali pa kupata mengi sio?
Nilikuwa nimekaa na wamama Fulani wenye uzoefu mzuri tu ktk maswala ya ndoa, wakitoa ushauri, nasaha, maonyo n.k kwa binti aliyekuwa akienda kuanza maisha mapya ya ndoa ili akawe mke mzuri.
Kama kawaida yangu mimi ni mtu wa kudadisi na kuhoji mambo mengi ila ngono ndio hunivutia zaidi, hivyo nilitaka kujua ngono ikoje kwa wanawake hasa kwenye maisha ya ndoa au niseme ndani ya ndoa.
Wachache walikuwa sio wazi sana kama kawaida ya wabongo wengi hasa watu wazima (nadhani waliona mimi katoto Fulani hivi kumbe ni kamwili tu haka)……nilivyoona wanadengua nikahamia kwa kwa wanawake vijana lakini walio kwenye ndoa na kuuliza tena “wao kama wanawake ngono ikoje ktk maisha ya ndoa?”.
Kila mtu akatoka na majibu yake kutokana na uzoefu wake lakini nilivutiwa na maelezo ya wale ambao waliolewa wakiwa bikira, wale wanaotumia madawa ya kuzuia mimba na wale wanaosukumwa/lazimishwa kufunga kizazi baada ya kupata watoto fulani…….
Nikapata jawabu kuwa wanawake wengi ni “victim” ndani ya ndoa/uhusiano wa kimapenzi bila wenyewe kujijua…..nasema hivyo kwa sababu zifuatazo:-
Akizaliwa ni binti wa mzee Fulani……..Akiolewa anakuwa mke wa Fulani…….Akizaa anakuwa mama Fulani…….alafu akijaaliwa nakuwa bibi fulani anamalizia na swala zima la kukabiliana na kukoma hedhi…..Kila hatua ya maisha yake mwanamke anakabiliana na majukumu lukuki……mwanamke huyu hajawa na nafasi ya kuwa yeye na kufurahia maisha kama yeye bali siku zote za maisha yake amekuwa akiishi kwa ajili ya watu wengine.
*Hebu tumuangalie mwanamke huyu anapofunga ndoa/ingia kwenye uhusiano…..
1)-Mimba usiku wa harusi (usiku wa kutolewa bikira).-Mwanamke kafunga ndoa akiwa bikira na kwa bahati mbaya au nzuri wanashika mimba usiku huo au wakati wa fungate…….binti huyu hajui lolote kuhusu ngono wala utamu wake….usiku huo anafanywa kwa mara ya kwanza na mume wake anajisikia safi kuwa mkewe hakuguswa na mtu mwingine bali yeye….
Hisia za kumiliki zina mjia na bila kujali maumivu ya binti yule, haki yake ya kupata utamu au kufurahia tendo la ndoa….mume anajimalizia ndani kwa vile tu ni mke wake.
Baada ya miezi 9 mwanamke anajifungua anaanza kukuru kakara za malezi na kukabiliana na mabadiliko kutoka msichana kuwa mama…..mabadiliko haya huwa ni magumu sana as u can imagine.
Kwa vile mwanamke huyu hajui lolote kuhusu ngono na hakuwahi kufundishwa au ambiwa lolote hukusu maswala yamwili yeye anachukulia au kuamini kuwa kilichofanyika au kinachofanyika ni kawaida……binti anahisi kuwa labda anakasoro kwani akikumbuka huko nyuma aliwahi kusoma, sikia, kuambiwa kuwa ukifanya mapenzi unasikia utamu au raha…..au anaona mumewe anavyofurahia….lakini masikini yeye haijui na wala hajawahi pupate utamu huo.
Mwanamke anashindwa ku-share na watu wengine kwa vile anadhani hiyo issue ni nyeti sana na ni kinyume na maadili ya kitanzania au mila na destru za kwao…..hivyo maisha yanaendelea na watoto wanaongezeka hali inayoongeza mabadiliko ktk mwili wake na sasa kila unapofanya mapenzi yeye ni kilio tu kutokana na maumivu (kwa vile hapati hamu ya kungonoana wala utamu wake) hali hiyo inamfanya mwanamke huyu amkwepe mumewe kwa kutafuta sababu nyingine……..
Mwanamke anaenda kulalamika kwa Daktari wake wa Magonjwa ya kike na anafanyiwa vipimo inagundulika kuwa mwanamke huyu anaelekea kwenye kukoma hedhi au kikomo cha hedhi (Menopause) kwa mwanamke huyu wa kibongo aliye ndani ya bongo kupata hamu au utamu wa kungonoana ndio inakuwa basi tena……na she is only 40yrs old.
*Ofcoz huwezi kutegemea binti wa watu bikira awe akitumia madawa ya kuzuia mimba au akujie na Condom ili azuie mimba…….wewe kama mwanaume chukua jukumu la kujizuia ili usimtie mimba binti wa watu ambe hajui chochote kuhusu unachokifanya……
Hili halitokei kwa Bikira tu bali kuna wale wanawake ambo walibakwa hivyo kisha wakaja funga ndoa, wapo walijiingiza kwenye maswala ya ngono wote wakiwa bikira hivyo hawakujifunza kitu, vilevile wapo waliokuwa kwenye uhusiano na wanaume ambao hawajali hisia za mwanamke bali tama zao za mwili….nakadhalika!
***********************************************Waendesha "Kitchen party"......tumieni wasaa huo kuwa wazi zaidi na kuwaeleza/andaa hao watarajiwa watarajie nini ktk maisha yao ya ndoa, jinsi ya kukabiliana baada ya kujifungua......sio mnashupalia jinsi ya kumfurahisha, heshimu, pika mahanjumati, kuwa sexy (pendeza na kuvutia @all times) na kum-keep mume......there are more than hayo in any relationship.....kumbukeni kuwa mwanamke anabadilika jinsi miaka inavyokwenda.....huyo binti anahitaji kulijua hilo kwa undani zaidi.
Wapenzi wanaume.......jaribuni kuvuta muda na mshirikishe mwanamke umpendae kwenye swala zima la kuzaa…..pangeni na muelewane mzae baada ya muda gani…..ondoa “umilikikaji” kumbuka huyo ni mkeo lakini pia ni mpenzi wako……mpe nafasi ya kuujua mwili wake kabla haujabadilika.
Kaka zangu hebu chukua jukumu la kuzuia mimba badala ya kumuachia mwanamke, kumbuka kuwa yeye mayai yake hayatoki lakini mbegu zako zinatoka na kumuingia kwenda kujenga kiumbe hivyo wewe ndio mwenye ku-control hilo na sio yeye.
Ni vema kujadiliana au kujua kama mkeo/mpenzi wako yuko tayari kukabiliana na mabadiliko yanayohusisha uzazi, kumbuka kuwa kuoa au kuwa na mpenzi sio tiketi ya kum-mimba mwenzio (cum inside).
Wanawake.......ambao mnaamini kuwa kupata mimba au kuzaa na Fulani basi ndio utapendwa zaidi au kutoachwa…… nakushauri uache huo Ujinga na Ushamba…..
Only Kubali kushika mimba ikiwa unadhani kuwa ndio kitu unachokitaka, hakikisha unajua faida, hasara, matatizo ya mimba mpaka kujifungua na baada ya kujifungua, kuwa na uhakika kuwa utakuwa tayari kukabiliana na yote hayo.
Epuka kukimbilia kuzaa/achia mimba kwa vile jamii inakukandamiza/sukuma, mtaani kwenu kila binti anamtoto, unahofia jamii kukudhania kuwa wewe ni tasa, ili wakwe wakupende zaidi, ili mwanaume/mume asikuache au aendeleze huduma kiuchumi n.k.....
Sikutishi….bali nakwambia ukweli kuwa kushika mimba maana yake ni mabadiliko…….je unauhakika uko tayari?
Tuende na wakati sio ktk mikao na mitindo ya kufanya ngono tu bali kila kitu kinachoendana na ngono na matokeo yake......tujaribu kuwa Taifa lenye vijana wajanja ei!.....sio tunapelekwa pelekwa na kasumba za kizembe.
Endelea kuwepo ili nimalizie vipingele 2 vilivyobaki….
http://dinahicious.blogspot.com/
0 Comments:
Post a Comment
Subscribe to Post Comments [Atom]
<< Home