Friday, December 7, 2007

MILA ZA WAMASAI NOMA SASA...ITAWAUA WENGI HII..

WAMASAI ni kabila moja kubwa sana, na ni kabila moja ambalo limekuwa likijitahidi kuenzi na kudumisgha mila na Destutri ya kabila hilo hapa nchini. Licha ya kufanya hivyo wa mila zao wamekuwa wakidumisha kwa staili ya ajabu hebu kaa mkao wa kula ushangae ya Musa. MILA hii katika kabila la kimasai inawalenga vijana ambao wamekwishaoa ambao rika lao linaitwa MORANI. MILA hii iko hivi yaani MORANI wa kimasai anapojisikia kufanya Ngono anakwenda katika nyumba yoyote ambayo ni kijana mwenzee mwenye mke. Kabla hajaingia ndani ya Nyumba hiyo anachomeka Mkuki wake mlangoni halafu akiingia ndani anamkuta mama mwenye nyumba wanaanza kufanya Mapenzi. Kila mtu anajua kuwa umasaini hakuna mipira ya Kiume yaani (condoms) wanashughulika bila kutumia zana ya aina yoyote hapa. wakati wakiwa ndani wanafanya mambo hayo Baba Mwenye Nyumba akija anakuta Mkuki uko nje ya Nyumba yake anachofanya ni kuondoka zake na kuwaacha Adam na Eva wanafaidi Tundi. Unajua akitoka hapo anakwenda wapi? akitoka hapa na yeye anakwenda katika Nyumba nyingine ambayo ana uhakika akienda atafanya kile ambacho mkewe anafanyiwa anafika anachomeka Mkuki nje anaanza kuvunja amri ya sita bila zana!!!!!!!!!!1 Sasa fikiria ni wamasai wangapi wapo Jijini Dar Es Salaam wanafanya kazi ya Ulinzi na wafanya Ngono na machangudoa wa kule Kinondoni kwa pesa ambazo wanapata. Wakirudi umasaini wanagawa Virusi bila kujua kuwa wanavimiiliki ndani ya miili yao kwa wake wa wenzao ambao nao watavipata bila kujua kwa wake wa wenzao. Kamchezo kazuri sana lakini kamejaa rafu za ajabu, yani hakuna refa wala mshika kibendera na mbaya zaidi hakuna hata wale wahudumu toka msalaba Mwekundu (RED CROSS), yaani ukichezewa rafu hakuna cha huduma ya kwanza wala nini! Sasa kama tukidumisha Mila zetu kwa staili hii ni nani atabakia katika Tanzania hii ambayo uchumi umekua kwa asilimia 4? Wakati umefika sasa tubadilike kuendana na Karne ambayo sasa ni Sayansi na Teknolojia na hatuko kabisa katika Zama za Mawe za Kale ati ee. NGO's, CBO's na Serikali hebu iangalie suala hili kwa ukaribu zaizi katatumaliza haka ka UKIMWI jamani kwa kudumisha mila kwa sataili hii. Sina hakika kama TACAIDS wana habari hii hebu walifuatilie basi hili jamani. TAKE CARE!

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home