Friday, December 14, 2007

Mlalahoi Anauliza: Nani Kakuloga WeTanzania?

Kuna maswali mengi uwa najiuliza, Lakini mada hii ya kutafakari miaka 46 ya uhuru, pengine naguswa na swali moja tu. Je kwa mfano naamka asubuhi najikuta au napokea simu nikiambiwa nimeteuliwa kuwa urais wa Tanzania hii tuliyonayo nitaanza na majukumu gani?Nina takribani miaka 35 sasa, najiona mtu mzima! Nikiangalia nyuma maisha yangu, naona kama ni miaka michache nimeingia duniani! Miaka 46 ya uhuru ni umri wa mtu mzima! Je mtu mwenye umri wa miaka 46 anaweza kufanya nini? Je huyu kijana au tumwite mzee wa miaka 46 bado anavalishwa chupi? je bado ananyonya maziwa ya mama? Je wazazi bado wanamvalisha nguo, wanamwambia Mr/mrs X nenda kapige mswaki! Huyu X bado anaomba hela ya kwenda kununua pipi? La hasha, hata nchi maskini kiasi gani, huyu X hawezi kuwa tegemezi kwa wazazi wake labda awe ana kilema cha maisha ambapo hawezi kujitegemea. Huu ni mri wa mtu ambaye sasa amekomaa, anaanza kumwangalia baba na mama, mama na baba sasa wanakuwa watoto, wanamtegemea huyu X! HUYU NINAYEMSEMA NI TANZANIA.Tanzania amekua, umri wa miaka 46 hutakiwi tena kuomba baba au mama yako eti nipe maziwa ninyonye! we Tanzania umekuwa mtu mzima. Nguvu, akili,na afya unayo ya kutosha kufanya kazi. Kitu gani sasa kinakusibu? Nani kakuloga we Tanzania?Majibu ni mengi miongoni mwa viongozi(yaaani mama na baba yako), eti utasikia wanasema " Mzungu alinifanya niwe kilema", wengine utasikia niilibiwa raslimali zangu, ningekuwa mbali!!!! lakini baba yangu WA KAMBO hasiti kusema na kurudia kauli yake ile ile eti KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI. ZIDUMU FIKRA ZANGU.Na hizi ndo FIKRA zilizomfanya tanzania awe hapa! umri umekwenda una miaka 46 sasa. Fikra za kuendelea kuwa maskini, fikra za kuendelea kwenda nyuma badala ya mbele.Nani alimloga huyu TANZANIA, je ni wazazi wake yaani wakoloni waliomzaa kisha wakaondoka, au wazazi wa kambo yaani CCM?Miaka 46 we TANZANIA umekuwa mkubwa, AMKA! AMKA! Amka wadogo zako uliozaliwa nao sasa wako mbali. Wazazi wako ingawa walikuzaa wakakuacha bila msaada (kama unavyodai), ujue wadogo zako akina Rwanda, India, Hong Kong nk wako mbali!Lakini cha kushangaza, hawa wazazi ingawa waliondoka si bado wanakupa hela ya kujikimu ingawa we mtu mzima! Nasikia hata baba wadogo zako akina IMF, WB,EU etc bado wanakupa hela ya kula! Ushibi wewe!Mh! huyu TANZANIA NASHINDWA KUM-DEFINE!Tanzania ana watoto lakini hela hawapi akipewa aitunze familia. Hata mali aliyoachiwa aitumie, hatuoni inaenda wapi?Hela unapokea, mali unayo sasa mbona UMEKONDA! Watoto wako wanadiriki kumfuata babu yao ngambo kuomba hela, we umekaa kimyaaa!.......Nitaendelea kumsema huyu Tanzania labda ngoja nisikie kaka na dada zangu wanasemaje........

0 Comments:

Post a Comment

Subscribe to Post Comments [Atom]

<< Home